NIFUTE MACHOZI.

Nifute machozi.

Dunia rangi rangile, hata tambara bovu hunufaisha kudekia,
Sisikie ukaambiwa, dunia tambara bovu, Leo iko hivi ,kesho iko vile.
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, haiishi dunia, wanaoisha Ni watu waliokuja kujiishia humu duniani.


Huhadaa, Tena Ni thamu, mfanowe sijaona, huwa thungu kiondoka mmoja , safari ya lazima isokuwa  na miadi.
Furaha zote muda huu huwa karaha.
Wata huambiwa, mtaondoka mrudi kwa Illahi Mola jaalia, mawazo hayo kila mtu mwenzie humwathia, Mimi huenda bado Niko , siku zangu hazijanifikia,
Hakuna aliendoka, akawa shughuli zake amejikamilishia.


Utawasikia waombolezaji, rafiki na familia, marehemu kaacha wanawe ubwabwa wa shingo haujawatoka, vipi duniani watajiishia, marehemu alikuwa ndio kwanza kaposa jamani Mola hakujaalia, kiwanja lichonunua ndio kwanza kaagiza matofali , Ya Mungu Ni mengi, ujue ya kuku Ni mayai, haya maisha na hii Dunia, haiko mnavyoidhania.
Furaha megeuka kuwa karaha.


Dunia huzungukia siku mbili, furaha na huzuni.
Yakupasa kuelewa, uingiapo furahani, fahamu ipo siku utakuwa mashakani.
Roho yenda mbio, hivi wana nini Hawa insani? Kila niingiapo sipendezi, kila nifanyalo lachukiza, nifanye nini mnione mwanadamu ? Ama ni hio kwamba maji mazito kuliko damu yangu? Ningekuwa mnajimu ningesema mnatembelea nyota yangu, kooni mmenisakama, Wallahi Sina amani.


Ningekosa Imani ningesema, nikamuulize yule ustazi aniangalilie Kama wasemavyo , hivi nakwama wapi?
Ayati lukuki zishatupa ufunuo, katika kurani tukufu, “Hakika mutaonjwa kwa uchache wa hofu na njaa, na kupata hasara katika Mali zenu, vifo, na kupoteza matunda ya juhudi zenu, Ila wapeni habari njema wanaosubiri na kuvumilia ; ” Wale wasemao, inapowakumba mitihani; Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake tutarejea. Hao ndio wapatao baraka kutoka kwa Mola wao, na huruma, na hao ndio wapatao uongofu.”

Kila lidondokapo chozi , fahamu , kunapokuwa na dhiki, faraja hupatikana papo. Hivyo shikilia kamba, wa kukufuta machozi ni Muumba, katu usichoke kumuomba shida zako zote. Amini atakufuta machozi.

KUWA UYAONE.

Nlipoambiwa kuwa uyaone nilidhani ni ghorofa. Ama niseme kama wasemavyo katika lugha ya kidigo, “Naambwa kula dze ugaone, nchigaona n’maembe mbaphi ni higa.” Yaani , niliambiwa kuwa uje uyaone nikadhani ni maembe kumbe ni haya. Kuwa uje uyaone, sio kwamba tulikuwa tunaapizwa, kuwa uyaone , ni huu ulimwengu, uliojawa na malimwengu ya hawa walimwengu.

Mtazamo wako wa ulimwengu unapokuwa mdogo ni sawia na mtu aliyehitimu chuo baada ya kusomea tajriba Fulani, hajapata uzoefu wa kutosha nyanjani, huenda nafasi za ajira zikampita, utawasikia kwenye vigezo wakitangaza kazi, lakini juu yake kutajwe na uzoefu wa miaka mitano hadi kumi. Sasa huyu anaejifunza kazi sasa hivi, kazi hio ataipata vipi?


Lakini unapozidi kukua, ndio fumbo linafumbuka, uhalisia wa maisha unaanza kuuona. Zile kauli za walimu ama mama nyumbani, “Ukijitahidi utafanikiwa.” Kumbukumbu zake zinakurudia kama Jana, unajiona mdogo, kama ulishabugi unauma kidole, laitani, ningalisikiza, laitani ningalikanyika pale mwanzoni nilipoambiwa.

Lakini , kwani maji ni mithili ya vumbi na taka, eti utafute kizoleo uyazoe, hukusikia waneni walivyonena, Maji yakimwagika hayazoleki ? Ama, majuto ni mjukuu huja baadae. Haidhuru lakini, ndio tathmini kamili ya maisha, hayana ramani , eti vipi utaishi, kwa makini pasi na kujikwaa ili upate furaha . Ni kama shilingi, maisha yana pande mbili, na yenyewe ni siku mbili ; moja ya furaha na nyingine ya huzuni.
Hakuna kipimo cha ufaulu ama kufeli.

Ukikaa hapo juu, usiwaangalie wenzio ukasema, “Hivi hawa wanakwama wapi? Watakua mabongolala, wameshindwa kujipa mwelekeo bora wa maisha?” Mafanikio yanalevya mno zaidi ya pombe au kilevi chochote. Mpanda ngazi hushuka, na wallahi haya ni mahesabu tu, juhudi haipiti kudura. Cha muhimu niwashauri na niendelee kujipa moyo, umri wa ujana ambao humpelekea kila mtu kuwa mtu anayetegemewa na familia yake na jamii kwa ujumla ni wakati uliojawa na changamoto mno.

Ndio wakati ambao wengi hukata tamaa, umejaribu mbinu kadhaa lakini juhudi hazifui dafu. Kubwa kuliko ni kwamba, hakuna ufanisi uliopatikana pasi na changamoto au uliokuja rahisi tu.
Changamoto ndio kuni zenye ushawishi, zinauchochea moto kuwaka na kukiivisha chungu kilichoko jikoni. Kubali kuzipitia changamoto, anguko lisikutie kiwewe, unapoanguka amka, katu usikate tamaa, siku yako itafika, Mungu hamtupi mja wake.

“Aluta continua” bado hatujafika lakini hatujaacha kwenda. Upweke unaokupa upeo wa kufikiri na kuvumbua vitu ni bora kuliko wingi usiokupa changizo chanya. Washike marafiki wanaokujenga, watu ambao wanafurahikia hatua zako pasi na nia mbaya au kukuonea gere na kukuchimba kupania kukupoka kile kidogo ulichonacho. Safari bado Ni ndefu, kazana, ni dhahiri umri huja na majukumu, na kupanuka kwa mtazamo wako wa maisha.

Kaa kitako peke yako, jiulize Mimi ni nani?
Niko wapi? Wapi ninaelekea? Hivi Dira yangu inanielekeza kuliko sawa katika ramani ya maisha yangu? Ukijidadisi na kujiswalisha? Ni jambo linalokupa msukumo, chachu ya maendeleo inaongezeka, uthubutu vilevile unajenga msukumo mkubwa, kwamba, iwapo sitaamka kulifanya hili ninalolitamani liwe, hakuna mjomba, shangazi au ami atakaekuja kunikwamua, msingi mkubwa ni mimi mwenyewe kujitoa kwa hali na mali , mbele ya safari nikihitaji msaada waje wanivute nilipokwama, aghalabu huo msaada pia unaweza usiupate , lakini Imani yako ya kujitoa kikamilifu ndio msukumo mkubwa wa viwango vya ufaulu.

Umuombe Mungu kila siku ilhali ukipigika na kutia juhudi, basi kwa kudura zake , atakufungulia. Usiishi chini ya vivuli vya watu. Muda wako mwingi ukautumia kupiga soga ama kwenye starehe, ama ukodolee macho simu janja, kukosoa maisha ya wasanii kwenye mitandao. Muda mwingi utumie kujidadisi, na kujipanga kwa ajili ya kuyakabili maisha.

Mnyonge Mnyongeni.

Nyie madhalimu, mnapopanga kuhujumu na kuzima ndoto zilizoshamiri katika vifua vya watu, mnabaki kucheka na kuona poa tu. Yenu yawaendea, wenzenu wakosekewa. Kwenu ni kama kubonyeza kitufe kwenye rimoti, kubadilisha chaneli moja kwenda nyingine katika runinga, hongereni.

Hivi hamjasikia, Mungu anasema hadhulumu, na ameiharamisha dhulma baina yetu insani? Ama mmesahau Kuna na siku ya malipo? Kwa Mungu hakuna majungu, mi nna Mungu. Niseme nitawashtaki nikatafute haki, naanzia wapi mie mtoto wa masikini, msikitu ? Haki imo mikononi mwenu, Sheria mnazibadili mtakavyo. Nguvu Sina, uwezo wa kuwapiku nautoa wapi?


Kimbilio langu ni Mungu. Nikisali nitaomba Dua, Tahajjud nitasimama na kulia, kwenye sijda sitaacha kujiombea. Mungu halali, Mungu wetu sote, atajibu , haikumpendeza abadani kunifanya mimi dhalili. “Nenda uendako, fanya ufanyalo.” Ndio kauli mzinenazo, kiburi kilichoshamiri kikakita mizizi, taji la Mungu mmelivaa nyie. Mnajiona hata riziki mnaweza mkaigawa nyie.

Walimbukeni wa umaarufu, na wavivu wa kufikiri. Mgawa riziki ni Mungu, na humpa amtakaye. Hizi mnazoshikilia nyie, na juhudi tuzifanyazo chini yenu, ni sababu tu za Muumba kutufikishia hio riziki. Kusimamisha kwenu sababu, hakujamaanisha ndio mwisho wa riziki toka kwa Muumba.

Mfahamu, mnatoa nafasi ya Mungu kukunjua mipango mingine katika maisha ya mja wake. Madhalimu mtakuwa nyie mumshinde Nani? Wamepita vigogo, firauni wa Misri aliyejiita Mungu, na wababe wengine wa karne mlizosoma katika vitabu vya historia, wapo wapi leo?

Hawako katika uso wa dunia, wamefukiwa na kusahauliwa, na kwa sasa wamebaki kumbukumbu tu. Mnacheza na Mungu nyie, badilini nyoyo zenu, hakuna atakaeishi milele. Iwapo mnaona bora tukadaiane tulipane huko kwa Maulana, maana ni mbali Sana, Sina budi kusubiria, maana huko kwa Mungu ndiko kwa hakimu wa kweli.

Hakuhitajiki hata Mawakili, ushahidi wote upo, utakwendawekwa parawanja. Nimejifunza, nakwenda, kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa upishi. Taratibu najikongoja, matumaini hayaishi.Mgawa riziki akeli hai, Anaishi.

Mtunzi: Omar Abdhallah. Kichwa Cha Habari: Mnyonge Mnyongeni.
Makala 01:Ndoto zilizoparanganywa.

TUNAUPENDA MPIRA.

Mpira, kabumbu ama boli kama unavyofahamika kwetu, ni kitu kinachopendwa kote duniani.
Kifaa cha tufe, kichezwe na watu ishirini na wawili, kumi na moja kila upande, au hata Saba, ama watu wacheze kando ya fuo za bahari almuradi tu wajipatie burudani ama wawe wanasakata kwa ajili ya kutafuta bora Ni nani.

Ndio utaona mpira una mashabiki wengi duniani, kila mmoja ana timu ama klabu aipendayo, anaishabikia kwelikweli, angalia hapa nyumbani, kama ilivyo Simba na Yanga, ama Gor Mahia na Fc. Leopards, ama ligi za uingereza, hispania, Italia na Ujerumani na nyingine kote duniani.

Mpira ndio miongoni mwa mchezo unaopendwa zaidi duniani. Waulize wanaopenda kabumbu watakujuza.
Kama hukucheza utotoni, cheza ukubwani. Huu mpira hautaki hasira. Mwanasoka moyoni, kabumbu sasa nalisakata ugani. Shabiki shakiki, mwenye ujuzi lukuki.

Nitokako wengi wanapiga kipute, wachache Sana mpira umewafaidi, hili ndilo linalonikata maini, talanta zinafia mitaani, hawajachezea hata daraja la kwanza, naanzaje kuitaja ligi ya taifa. Ila vipaji vipo, mbinu za kuvikuza na kuvipa thamani ya fedha ndio zimekuwa butu.

Angalia akina Ronaldo, Messi Rashford na wengine wengi waliotoka kwenye maisha magumu, talanta zao ziliwaokoa, Leo wanapiga hela Ni matajiri wasioshikika. Nikiwataja hao watajika wa mataifa ya mbali, huenda mkadhani mie si mzalendo ama hakuna wengine waliotajirika kupitia mpira Afrika, au hata hapa kwetu Afrika Mashariki.

Tunajivunia nyota tajika wa mpira duniani kutoka Afrika, kama Samuel E’to, Didier Drogba, Mohammed Salah, Sadio Mane, Paul Pogba,  na hata kwetu nyumbani , Victor Wanyama, Mbwana Samatta, na Michael Olunga, wote Hawa wametajirika kwa kusakata kabumbu kimataifa.

Nahisi kama wengine wamepigwa na butwaa. Kumbe mpira unalipa ? Ndio, tatizo miondombinu ya kutambua na kuvikuza vipaji, na nafasi za kutambulisha vipaji kwa vilabu vikubwa na ligi za nchi nyingine duniani haijafua dafu.


Mie nasakata kabumbu Kama ada, ama niseme ni kwa ajili ya afya bora, maana nikisema ni kupunguza uzito, mwili wenyewe umekauka , timbwili la maisha ni mazoezi tosha.
Iwapo Ni kukuza talanta, pengine sijajaaliwa, unajua Mungu hakupi vyote, na hupewi unachotaka, unapewa unachostahili.
Haya acha niingie uwanjani Mimi, kipenga kimepulizwa, nicheze mpira kuufurahisha moyo.

*Tumaini.*

Hii Dunia hivi unadhani tungeishi vipi kama sio kuwa na tumaini. Lakini tambua ulevi ulio mkali zaidi ni kulewa matumaini pasi na kuupa nafasi uhalisia, yaani utumainie kabisa katika jambo ila usiweke juhudi yoyote.

Na sisemi mimi, katika pitapita zako, na maisha ya kila siku, utakuwa umewasikia watu wana Ruwaza nyingi tu, utasikia Ruwaza ya elfu mbili thelathini (vision 2030) , mipango ya maendeleo ya dunia, muda mwingine watu wanapanga mipango hata ya kusudio la karne nzima. Hawana lingine wanalolitegemea bali ni tumaini tu.

Ni kama tunavyoamka asubuhi tukiamini kwamba siku itakuwa njema na yenye mafanikio, haijalishi hali zetu, mama alikuwa akiniambia siku zote nilipozongwa na mawazo na kumtaka ushauri; “Roho ni ya vyema mwanangu, usifikirie sana, tumaini kwa Mungu, kubwa ni amani ya moyo wako.”

Basi ni hilo tumaini linalotupa shavu, kama wasemavyo vijana wa uswahilini. Tunavimba wee, tunatuna wee, afya inatupa tumaini kwamba asaa kesho tutakuwepo hai na kuendelea kujukumika kuboresha haya maisha.

Ndio maana hata katika Quran tukufu tumeelezwa kwamba tusikate tamaa na rehema za Mungu, na kwamba Mungu anasamehe madhambi yote. Hivyo hata katika imani za dini, tunashajiishwa kushikilia na kuikumbatia tumaini, kwamba tunaweza kuwa watu bora katika matendo yetu ya kiimani, na katu tusijikatie shauri. Ila tumaini linalevya mno iwapo mtu hatajishauri kujifua bali akae tu, kusubiri mafanikio. Hakuna Jambo linalokuja pasi na jitihada. Lazima ujikongoje kisha baadae uinue mikono kumuomba Mungu akutilie baraka na fanaka katika juhudi zako. Natambua fika Jitihada haipiti kudura, ila  usitafsiri maneno haya, kwa uelewa wako pekee, pokea na mapokezi na uchambuzi wa binadamu wengine, bila shaka mitazamo ipo tofauti.

Ndio , tumeshaelezwa kwamba, hakuna jambo lililo hakika kama mauti. Lakini kila siku tunapanga mipango tukitarajia kwamba kifo hakitatujia karibuni, ndivyo tunavyojirubuni, ama niseme ndio namna ya kubaki na amani na akili razini tukifahamu fika hatutaishi milele, lakini ipo haja ya kujitumikisha  ili kuijenga dunia bora wakati ambapo tutakuwepo hapa duniani. Ndio tumaini tunalolishikilia pasi na kubughudhiwa na matukio mengi ambayo huenda yakatukatisha tamaa na kututoa katika malengo na azma zetu. Lakini tukipanga kwa  muda mfupi Ni kama tunajirubuni,maisha ya dunia ni mafupi mno.

Kuna maisha baada ya kufa, ambayo ndio ya kudumu. Hivyo basi, tuandae njema zetu kwa ajili ya kesho akhera mbele ya Mungu. Ndio kufaulu kwa ukweli huko, tuishi maisha yetu tukikumbuka kurudi kwa Muumba na kumtaka msamaha kila tunapokosea. Hivi, tumaini letu litakuwa limekamilika.

Buriani Rais Magufuli.

Nimetamani niandike, daftari zimalizike, na wino wangu ukauke.
Kwa moyo mzito, natafuta maneno, lakini kifo ni kizito, hakuna kauli mwafaka, ya kukieleza .
Mauko ni kama mwizi, huchukua tukipendacho.

Baba, mjomba, babu, kaka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ama Kama tulivyopenda kukuita Mjomba Magu, tumepokea habari za tanzia kwa mshtuko, bado tunalia kwa sikitiko.

Kwa majonzi Alhamisi tarehe kumi na nane Machi elfu mbili na ishirini na moja alfajiri, habari ziliniatua moyo mno, ulifariki usiku wa tarehe kumi na Saba, nikatamani nisifanye kitu chochote, nikae chini nilie na kuomboleza, kumpoteza kiongozi wa kweli,kiongozi mwenye misimamo asietetereka, Shujaa wa Afrika.

Majonzi yalipokuwa yametanda, na milizamu ya machozi ilipokuwa ikichirizika , na kamasi nyembamba ziliponitoka, nikakumbukia maneno yako:  ‘Tumtangulize Mungu siku zote’.
Na kauli mbiu; ‘Hapa Kazi Tu.’

Nikafuta machozi na kupiga pua, nikakoga maji baridi na kujipa moyo. Nifanye michakato nikimbilie kwenye ujenzi wa taifa, Jembe umetuacha mkono, hakuna wa kuziba lako pengo. Falsafa zako tutazienzi milele, hukutushajiisha tuwe wavivu, bali tujipiganie kama waafrika nasi tufike kilele.

Tanzania yote tunaomboleza, Afrika mashariki , Bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla tumempoteza kiongozi shupavu.
Kazi zako zote na miradi uliyohakikisha imesimama itabaki kama kumbukumbu yako milele. Katu hatutakusahau, tutakuenzi mpaka siku ya Kiyama.

Wafisadi ulikuwa umewasimamisha damu, ufisadi ukapambana nao, na kuufanya haramu. Kasumba za mwenye nacho kupora mali ya umma na kuachwa huru ukazifanyia mageuzi, ufisadi ukaupiga kufuli, wote wakanyooka katika idara za umma. Mali za wafisadi zikataifishwa na mahakamani wakafikishwa.

Yote kuitetea Tanzania iwe Bora, wamachinga ukawapa vibali vya kufanya biashara zao mijini, wasihangaishwe wanapotafuta riziki.
Wanyonge ukawahurumia, elimu ya bure kuanzia chekechea hadi shule ya upili ukaianzisha, palipo kuwa na dhuluma , wanyonge ukawatetea haki waipate, tukakuita Rais wa wanyonge.

Ndege Bombardier ukatununulia, Upanuzi wa Terminal 3 uwanja wa ndege Dar-es-Salaam ukatufanyia, S.G.R ukatuletea, Stendi mpya mbezi Louis ukatujengea, Ubungo interchange ukatujengea na fly over Dar zikabobea, ukatupunguzia msongamano wa magari na vyombo vingine vya Moto, Stylers Gauge; Mradi mkubwa wa Umeme wa Julius Nyerere ukatufanikishia, Mfumo wa  uchukuzi ukaukweza, barabara na madaraja kwa wingi ukatujengea. Dar tukasema imekuwa ulaya, umeme hadi vijijini na uchumi wa saa ishirini na nne. Mwaka elfu mbili na ishirini, Tanzania ikaorodheshwa kama nchi iliyoingia kwenye uchumi wa Kati.

‘Tanzania ya viwanda’ kama ilivyokuwa kauli mbiu ya awamu ya tano, ukaifanikisha , kadri Mola livyokuwezesha. Sekta ya madini ukaisimamia, wawekezaji wasipate kurubuni uchumi, walipie ushuru, na pia wachimba madini wazawa, wakapata vibali na idhini ya riziki kujitafutia.

Maradhi ya Corona Mola alitulinda , ukasema tushikilie maombi huenda tukapata salama
‘Lockdown’ ukaipinga, kutufanyia ahueni wanyonge, ulifahamu umasikini wetu, na njaa ingekuwa janga kubwa kuliko corona.
Mola litupa tahafifu mwaka ishirini ishirini tukaumaliza pamoja.
Umeondoka Rais wetu tutakuenzi siku zote.

Mola akupokee na akueke peponi palipo na wema, umeondoka duniani Ila athari yako imebaki nyoyoni. Umetufunza mengi, mapenzi ya kweli ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ulitoa sadaka maisha yako, kwa ajili ya watanzania na Tanzania.
Kazi ya Mungu haina makosa, hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake tutarejea, kifo ni haki, na kila mmoja wetu atayaonja mauti.

Pumzika salama Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,  Msomi wa kemia, kwa hakika dunia umeitibia, japo hukutuchoma sindano, tulikuita daktari Magufuli ,shahada ya uzamifu ulipojipatia, Tulijivunia Sana uwepo wako,ulikuwa zawadi kwetu iliyotoka kwa Mungu, athari yako itabaki milele.

*Shairi* – Buriani 
Magufuli.
Malenga -Omar Abdhallah Kimwaga.
Lakabu – *Malenga wa Dunia na Akhera.*
*Malenga Wa Diani.*

MBONI YA JICHO LANGU.

Ningasema, waja ‘ngenena, Looh! Sivyo ajisifiavyo. Na tena ajishauwa na kujitia hamnazo. Dunia hailele, na mwanzo wa ngoma ni lele, wanadamu huwawezi awawezaye ni Mterehemezi.

Neema zake Muumba hazihesabiki, na kumshukuru kwazo ndio maamrisho, kuwa mkishukuru Mola tawazidishia, Ila mkikufuru adhabu yake huwa Kali mno.
Mtoto ni neema kubwa , na Mola hajamjalia kila liyemuumba.

Watu huzunguka kwa matabibu na madaktari, angalau kuona wamepata sahali.
Wengi hukubaliana,alipangalo Mungu, halipanguki kamwe, nao huzidisha juhudi kumuomba awaruzukie, Kwa Imani ya Ile kauli ya Muumba, Niombeni Nitawajibu.
Wanawake wapo walio tasa, na wanaume wagumba, hutamani wanapoona wenzao, kifurahika na makinda, lowaruzuku Jalia.
Lakini kiwa Mungu hakuitikia, hata wakaishi miaka mia, wakenda mbio kujitibia, hawapati katu riziki ya mtoto.

Walinisema watu, na majungu kunipigia, ndoa meingia, lakini watoto hajajipatia.
Waja hawakosi la kunena, riziki hutoka kwa Maulana, akipenda nami ataniruzukia. Mara kadhaa nilikaribia Ila Allah hakunijalia.
Siku ilipofikia, miezi ikatimia, mitihani yote Rabbi akaniepushia, walo nitakia kheri ,mikono wakanyanyua kwa Jalali kuniombea.
Rabbi nijaalia nami, angaa masikio yangu yapate kufurahika. nikamzaa salama wa salmini, nimuite nani Kama sio ‘Mboni ya jicho langu’, ama ‘Fadhili’ baraka iliotokana na Mola wangu.


Waswahili walinena, Mboni ichafukapo,Jicho huwa mashakani, kila siku niombapo kwenye dua zangu hakosekani, na Wala sijawahi kuacha kwa Mungu kutoa shukrani. Kwani Rabbi hakunijaalia, mwana mwengine duniani. Japo nilihatajia ila hakuna wa kumpinga Manani.

Nikumuangalia mwanangu , moyo hutulia, ndio pumbao langu, Rabbi alonijaalia, ni yeye mmoja kama mtima, kwangu hakupata ndugu , ndivyo alivyopanga Darahima. Nakupenda mwanangu, umri umekwenda, mwana mwengine sikujipatia. Ningaitwa mama, ni wewe wangu Omari Abdhallah Kimwaga, Mola alienijaalia.

Siku zote za aushi yangu, mwanangu takufurahikia, nitapambana kila mbinu , kukupa unalohitajia, Allah mekukukuza , Leo hii najivunia.
Mungu hakupi kilema, akakunyima mwendo, wallahi nilitotoa nikahisi wanavyohisi insani liojaaliwa na Mungu kabla yangu.


Furaha ilioje, huyu mwana ndie mboni ya jicho langu.
Wewe ulieshika tama, usojua hatima, Muombe Karima, ikiwa Ni kheri mtoto atakujaalia, sikufuru ukenda kwa wanga, kuwataka msaada.
Simama kwa jaalia, kwa lolote unalohitajia, ikiwa Ni kheri kwako, Mola atakuitikia.

Shairi :*MBONI YA JICHO LANGU*. Mtunzi: Omar Abdhallah Kimwaga. Jina la Majazi alopewa na wazazi: Fadhili. Lakabu: Malenga Wa Diani. Malenga wa Dunia na Akhera.

Tungo hii ni maisha halisia ya mtunzi , ameandika muandishi kufikisha ujumbe wa mamake mzazi ambaye alibahatika na mwana mmoja tu.

Nakupenda siku zote za aushi yangu, mamangu Mariam. Mwanangu wa kwanza kipenzi Mungu akinijaalia wa kike.❤️🤗♥️♥️

Diego Armando Maradona. ( Icon: but above all a human).

When Diego Armando Maradona passed on , on Wednesday 25th, 2020, it was a sad day for football fans all over the world. The world had lost a great footballer, an icon, who loved football and played with great passion and enthusiasm. A man who through his love and commitment for the sport, inspired millions to play football but most importantly hold on to hope. From the Slums in Buenos Aires, Argentina . To stardom, winning the world Cup and other accolades around the world is not a chance story. There was hardwork and luck from God.

But for me, the most important thing in his life , would be, his low point, where he fought Great drug addiction and seemed to be losing his Superhero stature in front of the world’s watch. Amidst all this he stayed an awesome human being, he showed the world that beyond the successful footballer and icon, he was as vulnerable as everyone of us could be.

He lived through his low moments and acknowledged the bad choices and mistakes he made over the years because he was a human being. It’s alright to go astray at some point because life could be overwhelming and none of us whatsoever has the right grip on it. Sometimes things happen beyond our control. But the best thing is always to stay positive and bounce back even amidst life difficulties.

RELATIONSHIP ADVICE. -01

When people talk about being raised by mothers, most of the people in society view men as irresponsible and uncaring in this context. They don’t ask from these men to hear their stories.

Some of these women were left because they were uncontrollable, vulgar , cheats and all sorts of bad things. That’s why they choose to feed their children with all sorts of negative energy to men figures in society or rather their absent fathers.

I don’t rule out that we also have rogue, irresponsible men, who walk out of women after impregnating them , in a bid to avoid the responsibility and stay young to keep doing their womanizer stunt, and others who are abusive and unfaithful leading to marriage and relationship break ups, these ones should also be shamed and talked about.

Mind you, we also have men who have taken care of their children from a young age to the time they become adults in a single parent family. This men stood out and Sacrificed themselves to ensure their children never lacked anything and they played the roles of a father and mother.

Don’t just victimize a whole Sex, for a single act of relationship gone sour, don’t be mean to poison your children about the partner you had a relationship with that led to them being born. Because you’d only brainwash that child and feed him or her hatred putting him away from your fellow parent for the rest of his life. We acknowledge the single Parent families headed by either men or women for some reason or the other .

Nobody wants to be found stuck in an abusive relationship that’s not working out, we all want peace in our lives. But be true to yourself, don’t demonize your fellow parent because you want to win the heart of your children, let the misunderstanding be for you adults, and of course find a balance for your hurt and hatred to put your children first. In this way, we will reduce the number Of broken marriages and Relationships in future.

Teach your children the importance of forgiving, loving, and making marriage relationship work in future but of course avoiding being hurt in the name of loving an individual.

Researchers In Madina Find CoVid 19 treatment.

Who Is Muhammad?
Prophet Muhammad is the Last Prophet in the Religion of Islam, and this blog site will help you to learn more about Islamic news daily and

Researchers in Madina find successful COVID-19 treatment – The City of the Prophet

As we all know that the city of Madina in Saudi Arabia is close to the hearts of every Muslim because the noble Prophet of Islam, Muhammad (PBUH) is resting in that city along with thousands of his companions and family members, even two of his very close companions Hazrat Abu Bakr Siddiq (RA) and Hazrat Umar Farooq (RA) are also resting with the noble Prophet Muhammad (PBUH) in the same chamber at Masjid Al Nabawi in Madina.

NEWS: Medical Researchers team in Madina of Taibah University, Madina Al-Munawwarah, Saudi Arabia find a successful treatment of COVID-19 as the team of these researchers treated patients of COVID-19 and their contacts with a regimen that have black seeds (Nigella Sativa), which according to a hadith of the Islamic prophet Muhammad (PBUH) has a cure of all diseases except death.

Prophet Muhammad Told The Medicine to Cure Coronavirus 1400 Years Ago, Now Approved by US – FDA

The hadith is of Sahih Grade (authentic):

The prophet (PBUH) said: “Use the Black seed for Indeed, It is a cure for all diseases, except death”

  • From (Sahih al- Bukhari)

Narrated Abu Huraira: ” The Prophet said – there is no disease that Allah has created, except that he has also created its treatment (cure).

From- Volume 7 Book 71, Number 582 Sahih al- Bukhari

The researcher’s team paper regarding the use of Black seed and Chamomile has been published in the American Journal of Public health and research and made public for everyone to look it own their own.

Let us more focus on what our noble Prophet said about the use of Black seed as medicine:

Aisha reported: The Messenger of Allah, peace, and blessings be upon him, said, “This black seed is healing for all diseases but poison.” She said, “What is poison?” The Prophet said, “Death.”

Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 5363

Grade: Sahih (authentic) according to Al-Bukhari RECOMMENDED DOSAGE OF BLACK SEED & CHAMOMILE

One dose of TaibUVID* consist of:

  • 1 teaspoon (2 grams) of black seeds
  • 1 teaspoon (1 gram) of {ground} chamomile
  • 1 teaspoon of natural bee honey

Mix well, chew well & swallow it, to give your mouth a refreshing taste drink some lemon drink or orange juice after drinking or consuming the above-mentioned medicine (ORANGES & lemons contains antioxidants and Vitamin C) gives you a different taste and will boost your immunity too.

*TaibUVID stands for Taibah University anti-COVID-19 treatment.

Prevention:
Take one dose [of the above] daily, until this epidemic ends.

Treatment:
Take five doses daily, for an entire week.
Then take one dose daily until the epidemic ends.
If there is severe cough or difficulty in breathing, you can inhale the vapors from black seed oil, or clove oil, or what remains of the solution after boiling [and sifting] black seeds and chamomile.
Simply place any of the above in a nebulizer, and inhale [the vapor].

If you do not have a nebulizer, then you can put one tablespoon of black seeds, one tablespoon of chamomile, and one cup of water in a pot, and cover it partially.
Then, let it heat on low heat and inhale [the vapors]. Do this 5-6 times a day.
According to the paper published by the Department of Clinical Biochemistry and Molecular Medicine, Faculty of Medicine, Taibah University, Madinah, Saudi Arabia:

“We studied the effect of natural plants which are well known and which scientific research has shown [to be effective in this], such as black seeds (Nigella Sativa), chamomile (anthemia hyaline), and cloves, in order to treat the Coronavirus [Covid-19].
[…] both black seeds and chamomile can completely stop the growth of the Coronavirus.”

Dr. Salah Mohammed El Sayed head of a team of ten researchers said:

“By Allah’s favor, all of the Corona [Covid19] patients who used this treatment, TaibUVID, have improved, and they prepared it in their own homes. It did not take a patient for more than one week to improve.”

“We have published the therapeutic protocol in a medical journal so that everyone can access it. Perhaps we can save the life of someone dear, and how many they are! Allah knows the intentions. By Allah’s grace, all cases have recovered. May Allah protect everyone. O Allah, I have relayed [this information]. O Allah, bear witness,” he said.

Black seeds (Nigella Sativa) and chamomile (anthemis hyalina) were confirmed to inhibit coronavirus replication maximally. In addition, black seeds enhance immunity, exert tissue-protective effects, and effectively treat co-morbidities.

Pure honey taken orally exerts potent antiviral effects, enhances immunity, and exerts tissue-protective effects.

According to the researchers: “Our suggested TaibUVID and TaibUVID Plus are promising evidence-based approaches to save lives and decrease the death rates.”

Medicine approved by America – FDA as a preventive medicine which is ” hydroxychloroquine” is a derivative of thymoquinone (TQ), which is the component of the Black Seed ( Nigella Sativa/ Kalonji seed) and guess what?

It was told us 1400 years ago (in a hadith) that this black seed is a cure to all illnesses except death. Like every other scientific prediction, that has never been wrong of our Prophet Muhammad (PBUH) this one is also not going to be one because already Food & Drug Administration in the United States and ICMR in India has approved this medicine to be given to those who are at high risk of COVID-19.

Share
19 comments:

HYDERALI PM14 June 2020 at 06:15
A good information

Reply

Mihn14 June 2020 at 10:39
Please clarify, it is the oil of blackseeds or the seeds itself mix with chamomile ground leaves and honey together?

Reply
Replies

RAEEZA14 June 2020 at 14:07
Black seeds.

Reply

Unknown14 June 2020 at 14:26
Alhamdullilah, I was a covid-19 patient and proved that Black seeds with Honey/ black seeds boiled in hot Water and drank for 10 days . Now I am completely cured and healthy Alhamdullilah

Reply
Replies

Unknown14 June 2020 at 14:27
I am from Madina Munawara

Unknown14 June 2020 at 15:53
how many volume of black seeds?

Unknown14 June 2020 at 19:03
Hoeveel keren dronk u het per dag

Unknown14 June 2020 at 22:00
Alhamdulillah

Reply

Unknown14 June 2020 at 17:47
Truth Will always prevail

Reply

Abdulazeez Anifowose14 June 2020 at 18:09
Let the WHO acknowledge this and spread the news na

Reply

Unknown14 June 2020 at 18:14
Pls can black seed and honey cure ulcer,if true pls someone should explained how yo use for me

Reply

Murad14 June 2020 at 19:42
Licorice root as a powder or pills will cure ulcer Insha’ Allah. Many people will take spoon full of its powder and mix it with 8-10 oz water.
Any form of the licorice will help. They even sell it in form of pills at the Vitamin Shoppe in the US. https://www.vitaminshoppe.com/p/nature-way-licorice-root-450-mg-100-capsules/nw-1158

Reply

Ngondo14 June 2020 at 21:12
Alhamdulillah, it’s useful news.

Reply

Unknown14 June 2020 at 21:27
Where can I find chamomile in USA or Canada? Is it the flower or the leaf of chamomile plant we are supposed to use?

Reply

Mahfooz14 June 2020 at 21:35
Yes this is true. When I got infection with hapatatis c. I used to eat every morning after fajar Salah. Black sheeds with honey. And also I pray 40 time ya hafizun. Alhamdolilla I am totally cured with this deseas…

Reply

Unknown14 June 2020 at 21:43
It is a great news. Can someone please explain chamomile?

Reply

harisdaba14 June 2020 at 21:56
Masha Allah! The noble prophet (S.A.W) has always been right.

Reply

Unknown14 June 2020 at 22:01
Alhamdulilah good….I am consuming it daily in empty stomach and suggests my clients and friends too.

Reply

Jcboy tv14 June 2020 at 22:08
Masha’allah

Reply


Home
View web version

Powered by Blogger.

Design a site like this with WordPress.com
Get started